Je unawaza kujenga Nyumba, je unawaza uanzie wapi?
Kwa mtazamo tu kama huna uwezo wa kufata wataalam wakusaidie basi fanya hivi...
1. Tulia,na fikiria kuhusu mchoro wa nyumba unayotaka iweje kwa muonekano uupendao, lazima ujue mapana na marefu na kimo.
2. amua kuhusu material uyatakayo eg, aina ya mbao, tofali,milango na madirisha, cable za umeme, na kila utachopenda kiwepo.
3. from there unaweza kufanya makadirio kwani ukijua upana, urefu na kimo cha nyumba idadi ya matofali itapatikana, gharama ya matofali waweza survey ukajua then itasaidia.
4. bei za bidha zingine utatembelea maduka yanayohusika fanya window shopping, sio lazima ununue vifaa karibu na site yako what matter most ni final cost baada ya kufikisha site.
Na kwa wale wanaoeza kuafford, fanya hivi,,
Onana na wataalam in sequence as follows;
- Architect(Msanifu Ujenzi)
- Structural Engineer kama anahitajika! nina maana kama unataka nyumba yako iwe ya Ghorofa, kama si ya ghorofa si lazima structural Eng awepo!
- Quantity Surveyor.
Tuelewe maana ya simple house kwanza,
"simple house" ni affordable house ambazo ni nyumba basic na mara nyingi hazina vyumba vingi vya kulala, ni kama viwili, au zaidi sana vitatu kwa kuwa ukubwa wa nyumba kwa maana ya eneo lina uhusiano wa moja kwa moja na gharama za ujenzi bila kujali nani anajenga, wapi inajengwa wala material yanayotumika. kwahiyo ikawa una nia ya kujenga nyumba ya bei nafuu lazima uanzie kwenye ukubwa wake! then mengine yanafuata.
Rule of thumb!"500,000/square meter
Construction cost=Urefu X Upana X 500,000
Nikiimaanisha Square meter za ramani yako times 500,000(hii haina uhakika 100% but can be used as a guiding tool)
Siku Njema..
C...
0 comments:
Post a Comment