Hii nimetoa facebook,
Eti kun ukweli ndani yake???
Kauli 8 ambazo mwanamke akizitoa
jihadhari sana
1. Mwanamke anaposema, 'sasa hivi' au 'dakika moja tu,' maana yake ni
kwamba, ni nusu saa ijayo.
2. Mwanamke anaposema, 'utajua mwenyewe,' ana maana kwamba amekasirishwa na kukatishwa tamaa na tabia yako na sasa hajali tena.
3. Mwanamke anapopumua kwa nguvu, yaani kushusha pumzi kwa kishindo, hiyo pia ni kauli kwa upande wake.
4. Mwanamke anaposhusha pumzi polepole, ina maana kwamba, amekubaliana na wewe.
5. Mwanamke anapotumia neno, 'sawasawa,' kwa kawaida kama kuna jambo umemfanyia, ina maana kwamba, 'ninachukua muda kutafakari, halafu utaona nitakachokulipa baadaye.
6. Mwanamke anapotamka neno, 'we endelea tu,' anakuwa na maana ya kwamba, siku si nyingi zijazo, atafanya jambo ambalo hutalifurahia, kama hutaacha kufanya kitu au jambo lenye kumuudhi.
7. Kuna wakati mwanamke anaweza kusema, 'sawa bwana fanya,' kama kuna jambo ambalo hamjafikia muafaka au amebaini umekuwa ukifanya jambo fulani baya au lenye kumkera. Hapa hana maana kwamba, amekuruhusu kwa moyo mmoja,
8. Je kama mmeshindana katika jambo au umemkera katika jambo au mambo fulani, kutokana na tabia au mwenendo fulani, halafu akakumabia, 'asante sana,' itakuwa na maana gani? Hii ina maana umemkera kupita kiasi na bado wala hajajua akufanye nini.
hehhe...
Kutoka Facebook
Posted by
Unknown
|
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment